Tottenham Hotspurs kuikabili Ajax Amsterdam

0
372

Mchezo wa mkondo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya,  unachezwa  hii leo Kaskazini mwa jiji la London nchini England.

Katika mchezo huo Tottenham Hotspurs itakuwa nyumbani kukipiga na Wadachi, – Ajax Amsterdam ambao wamekuwa tishio baada ya kuviondosha vigogo viwili ambavyo ni  Real Madrid na Juventus Turin.

Akizungumzia mchezo huo,  kocha wa Tottenham Hotspurs, -Mauricio Pochettino amesema kuwa hawana cha kupoteza kwa sababu tayari wameshatimiza ndoto yao.

Hii ni mara ya kwanza kwa miamba hiyo ya Kaskazini mwa jiji la London kufika hatua hiyo ya Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya na kocha huyo Muargentina anasema kuwa tayari wameshatimiza ndoto yao ila wanafikiria kwenda mbali zaidi.

Pochettino anaelezea mafanikio ya timu yake kwa kusema kuwa kama umefakiwa kitu fulani kwenye maisha basi ujue ulishakiotea awali na kwamba wao kufika hatua hiyo ya Nusu Fainali ilikuwa ni ndoto yao tangu miaka mitano iliyopita .

Na akamalizia kwa kusema kuwa ili uweze  kufika mawinguni kwanza lazima uanze kuota kufika mwezini na hapo ndio utafika mawinguni.