Timu ya wanaume JWTZ yapongezwa

0
157

Mkuu mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas ameipongeza timu ya mpira kikapu ya wanaume ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kwa kuwa miongoni mwa timu bora za majeshi duniani.

Kanali Abbas ametoa pongezi hizo wakati anafungua kikao cha kamati ya utendaji ya Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMMATA) kinachofanyika mkoani Mtwara.

Katika michezo ya majeshi ya dunia ya mpira wa kikapu iliyofanyika nchini Ujerumani, timu hiyo ya wanaume ya JWTZ ilifika hatua ya nusu fainali, ambapo kati ya timu bora 23 za majeshi duniani imeshika nafasi ya nne na kutoa mchezaji bora wa mashindano.