Timu ya kriketi ya Tanzania yajinoa kwa mashindano ya dunia

0
369

Timu ya Taifa ya Tanzania ya Mchezo wa kriketi ipo kambini jijini Dar es Salaam kujiandaa na mashindano ya kufuzu fainali za Afrika yatakayowawezesha kushiriki mashindano ya dunia ya mchezo huo yanayotarajiwa kufanyika mwaka 2021 nchini India.

Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha Kriketi Tanzania, Shahid Dhanani amesema muamko wa wachezaji wa timu hiyo ni mkubwa, huku kocha wa timu Steve Tikolo akisema anaendelea kurekebisha mapungufu anayoyaona

Jumla ya wachezaji 30 wapo kambini wakiendelea na mazoezi ya timu iyo kwenye viwanja vya Annadir Burhan kwa ajili ya kujianda na michuano ya mchujo kwa ajili ya Kanda ya Afrika, mashindano yanayotarajiwa kufanyika Afrika ya Kusini