TFF yashauriwa kuzipa nafuu timu za ligi

0
1207

SHIRIKISHO la soka hapa nchini TFF limeshauriwa kuzipatia mgao wa fedha vilabu vya ngazi ya juu hapa nchi kutoka kwenye fedha watakazopata za FIFA.

Akiongea na TBC, Mkurugenzi wa Mtibwa Sugar Jamal Baiser amesema vilabu vingi hasa vya ligi kuu hali zao ni mbaya kiuchumi hivyo wakipata fedha hizo zitawasaidia kuendesha timu zao

FIFA Watatoa dola laki tano kwa kila mwanachama wake duniani kote ili kuwaokoa wanachama wake na mdororo wa kiuchumi uliosababishwa na janga la Corona.