Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limemteua Etienne Ndayiragije, kuwa Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Soka (Taifa Stars) kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Ndayiragije ambaye hivi karibuni alivunja mkataba wake na Azam FC, alikuwa kocha wa muda wa Taifa Stars tangu kuondoka kwa Kocha Mkuu Mnigeria Emmanuel Amunike.
Taarifa iliyotolewa na TFF imeeleza kuwa, uamuzi wa kumteua Ndayiragije kuwa Kocha Mkuu wa Taifa Stars umezingatia mapendekezo ya Kamati ya ufundi ya Shirikisho hilo ambayo ilipitia wasifu wa Makocha mbalimbali walioomba nafasi hiyo.