TFF: Waziri Dkt. Ndumbaro hajafungiwa

0
440

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limesema kuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro alishinda rufaa ya adhabu ya kufungiwa miaka saba iliyotolewa na uongozi wa TFF uliopita.

Ufafanuzi wa TFF umekuja kufuatia uwepo wa taarifa ya kuwa Dkt. Ndumbaro alifungiwa tangu mwaka 2017.

Kamati ya Rufani ya Nidhamu ya TFF chini ya uongozi wa sasa ilisikiliza rufani hiyo mwaka 2017 ambapo Waziri Dkt. Ndumbaro alishinda, hivyo kuondolewa adhabu ya kufungiwa,”- imesema taarifa ya TFF.

TFF imeongeza kuwa Dkt. Ndumbaro ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Rufani ya Leseni za klabu ya TFF.