TFF: Ndondo Cup haina kibali

0
222

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesema kuwa halijatoa kibali cha kufanyika kwa mashindano ya Ndondo Cup, ambayo tayari imesikia kuwa yanatangazwa kufanyika.

TFF imesema yenyewe ndiyo yenye mamlaka ya kutoa kibali cha mashindano yoyote yanayofanyika hapa nchini yanayoandaliwa na mtu binafsi au taasisi.

Hadi sasa imesema imetoa kibali kwa taasisi moja tu kuandaa mashindano ambayo yatafanyika katika kipindi cha mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan.