TFF: Maandalizi yapo sawa kuelekeza mchezo wa Yanga

0
159

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaendelea na maboresho ya maeneo mbalimbali ya Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa ajili ya mchezo wa Fainali ya Kombe la Shirikisho barani Afrika unaotarajiwa kuchezwa Mei 28 mwaka huu kati ya Yanga dhidi ya USM Alger ya Algeria.

Akizungumza na waandishi wa habari, Afisa Habari wa TFF, Criford Ndimbo amesema kama waliobeba dhamani ya michezo nchini wanamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwa mstari wa ambele kuhamasisha michezo nchini.

Ndimbo amesema maandalizi ya mchezo huo yote yanaendelea vizuri na hatua za mwisho za kukamilisha yaliyobaki zinaendelea.

Mechi ya marudiano itafanyika Algeria Juni 3 mwaka huu ambapo Rais Samia ametoa ndege itakayobeba timu na mashabaki kuelekea kwenye mchezo huo.