TFF inachunguza vitendo vya vurugu viwanjani

0
2055

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limekemea vikali vitendo vinavyoendelea vya baadhi ya Mashabiki kupiga Mashabiki na Viongozi wa Timu pinzani na kusema, Shirikisho hilo limeanza kukusanya ushahidi wa matukio yote ya aina hiyo kupitia CCTV camera zilizoko uwanjani.

kwa mujibu wa taarifa ya TFF, “Watu wote wanaohusika na vurugu kwenye mpira wa miguu (Mashabiki na Viongozi) watachukuliwa hatua kali za kinidhamu pia wote wanaotoa shutuma kwa Viongozi na maneno ya kuhamasisha vurugu katika mpira wa miguu nao watachukuliwa hatua kwa mujibu wa kanuni zilizopo”

Hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la matukio ya baadhi ya mashabiki kuwapiga mashabiki wa timu nyingine vitendo vinavyolaaniwa vikali na wadau wa soka