TETESI: Job awindwa Azam, Simba

0
144

Nyota wa kimataifa wa Tanzania, Dickson Job anaelekea kwenye miezi ya mwisho ya mkataba wake Jangwani na tayari timu kadhaa zinahitaji huduma yake.

Simba, wao wanahitaji huduma ya nyota huyo na tayari jitihada za haraka zimefanyika ili kuinasa saini yake, wameshaweka ofa nono mezani pamoja na mshahara ambao ni mara tatu ya anachopata hivi sasa, taarifa za uhakika ni kuwa Simba wanasubiri ‘account number’ yake tu.

Kwa upande wao Azam wameulizia upatikanaji wake na walichoambiwa ni kuwa kama wapo tayari kwa ajili ya mazungumzo basi wakutane ili watimize matakwa yake yote ya kimkataba, hili ni juu yake.

Huku hayo yakijiri, Yanga wamemwita na kuzungumza naye na wametaja dau lao (signing fee) na mshahara, ingawa inasemekana hajasaini karatasi yoyote ya Yanga mpaka hivi sasa.