Tembo warriors yaichapa Uzbekistan

0
142

Timu ya Taifa ya Watu wenye ulemavu (Tembo Warriors), imeshinda dhidi ya Uzbekistan kwa goli 2 – 0 katika mashindano ya kombe la dunia 2022 yanayoendelea nchini Uturuki.

Kwa matokeo hayo, Tanzania inasubiri mchezo kati ya Poland na Hispania utakaochezwa saa 12 jioni ya leo, mchezo utakaoamua nani kati ya Poland na Tanzania atashika nafasi ya pili katika kundi lao.