Tembo Warriors yachapwa na Poland

0
147

Timu ya Taifa ya Soka la Walemavu, Tembo Warriors, leo imepoteza mchezo dhidi ya Mabingwa wa Ulaya, Poland, baada ya kukubali kipigo cha 3-0. Poland ni mabingwa wa Ulaya kwa mashindano ya soka la walemavu 2022 na ni miongoni mwa waanzilishi wa mchezo huo.

Tanzania sasa itatupa karata yake nyingine kesho dhidi ya Timu ya Taifa ya Uzbekstan ambayo muda huu ipo uwanjani ikipambana na Hispania.