Tanzanite Queens nje Kombe la Dunia

0
1575

Timu ya Taifa ya soka ya wanawake ya Tanzania chini ya umri wa miaka 20, Tanzanite Queens imeondolewa katika kinyang’anyiro cha kuwania nafasi ya kucheza kombe la dunia nchini Costa Rica baada ya kubugizwa goli mbili kwa sifuri katika mchezo uliochezwa huko Addis Ababa, Ethiopia.

Tanzanite Queens imeondolewa katika michuano hiyo kwa jumla ya goli mbili kwa moja baada ya kupata ushindi wa goli moja kwa bila katika mchezo wa kwanza uliochezwa kwenye uwanja wa Amaan, Zanzibar.