Sven ajiunga na FAR Rabat ya Morocco

0
216

Aliyekuwa kocha Mkuu wa Simba Sven Vandebroeck, amejiunga na Klabu ya soka ya FAR Rabat ya nchini Morocco kwa mkataba wa miaka miwili.

Taarifa ya Klabu hiyo ya Jeshi la kifalme la Morocco (Royal Army) iliyochapishwa kwenye mitandao ya kijamii nchini humo imemuonesha kocha huyo akisaini kandarasi ya kuinoa klabu hiyo.

Sven aliachana na Simba kwa makubaliano ya pande zote mbili, lakini siku moja baadae ametambulishwa kwenye Klabu hiyo ya kaskazini mwa Afrika.

Sven ameiwezesha Simba kutinga hatua ya makundi ya Klabu Bingwa Barani Afrika kwa mara ya tatu, tangu kuanza kwa mfumo wa ligi ya ngazi za Klabu barani humo.