Stars yawekewa milioni 500 mezani ikifuzu AFCON

0
242

Rais Samia Suluhu Hassan ameahidi kutoa shilingi milioni 500 endapo Taifa Stars itafuzu kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2023.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Balozi Pindi Chana wakati akizungumza na wanahabari katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuelekea mchezo kati ya Taifa Stars dhidi ya Uganda, Machi 24, 2023 nchini Misri.

Timu hizo zitarudiana tena Machi 28 mwaka huu mkoani Dar es Salaam.

Mashindano hayo ambayo yatahusisha mataifa 24 ya Afrika yatafanyika nchini Ivory Coast Januari 2024.