Stars yang’ara mbele ya Malawi

0
203

Timu ya Tanzania (Taifa Stars) imeng’ara katika uwanja wa Benjamin Mkapa Mkoani Dar es salaam kwa kuichapa Timu ya taifa ya Malawi, ‘The Flames’, mabao 2-0 katika Mchezo wa kimataifa wa kirafiki ulio katika kalenda ya FIFA.

Baada ya dakika 45 za kipindi cha kwanza, Taifa Stars imepata Mabao yake kupitia kwa Mshambuliaji wake hatari John Bocco katika dakika ya 68 baada ya kumalizia kazi nzuri ya Denis Kibu na bao la pili likiwekwa kamabani na Beki Patrick Israel Mwenda katika dakika ya 75 kwa mpira wa adhabu ndogo baada ya Denis Kibu kuchezewa rafu karibu na eneo la hatari la timu ya Malawi.