Timu ya Taifa ya Soka (Taifa Stars), kesho itatupa karata yake ya Pili dhidi ya Libya katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2021 zitakazofanyika nchini Cameroon.
Stars ambayo itacheza mchezo huo wa ugenini, itakuwa na kazi ngumu baada ya kuumia kwa mlizi wake Erasto Nyoni ambaye amekuwa akitegemewa katika kikosi hicho.

Kocha wa timu ya Taifa ya Soka ya Tanzania, – Etienne Ndayiragije amesema kuwa, Nyoni ni mchezaji muhimu ndani na nje ya uwanja, hivyo kuumia kwake ni pigo kubwa kwa Stars.
Erasto Nyoni aliumia goti kwenye mchezo uliopita dhidi ya Equatorial Guinea, na hivyo kusababisha asisafiri na wenzake kwenda nchini Tunisia kwa ajili ya mchezo wa pili wa kufuzu kwa michuano ya AFCON dhidi timu hiyo ya Taifa ya Libya.
