Timu ya Taifa ya soka ya Tanzania (Taifa Stars) imefuzu kwa mara ya pili kwa michuano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN).
Taifa Stars imefuzu kwa michuano hiyo baada ya kuifunga timu ya Taifa ya Sudan mabao mawili kwa moja katika mchezo uliochezwa nchini Sudan.
Mchezo huo ulikuwa wa marudiano baada ya Sudan kushinda hapa nyumbani kwa bao moja kwa bila hivyo Taifa stars imefuzu kwa faida ya kufunga magoli mengi ya ugenini.
Hii ni mara ya pili kwa Tanzania kufuzu kwa michuano ya CHAN mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2009 kule nchini Ivory Coast.
Fainali za michuano hiyo ya CHAN itafanyika mwezi January mwakani 2020 kule nchini Cameroon na Taifa Stars itakuwa miongoni mwa timu 16 zitakazoshiriki michuano hiyo.

