Stars wako tayari kwa mpambano na Equatorial Guinea

0
1164

Kocha wa timu ya Soka ya Taifa (Taifa Stars), – Etienne Ndayiragije amesema kuwa, kikosi chake kina kibarua kigumu mbele ya timu ya Taifa ya Equatorial Guinea kwenye mchezo wa hatua ya makundi wa kufuzu kwa fainali za mataifa ya Afrika, lakini kipo tayari kufanya vizuri kwenye mchezo huo.

Ndayiragije amesema kuwa kikosi chake kimepata mazoezi ya kutosha ili kupata ushindi, nahodha wa kikosi hicho Mbwana Samatta na mlinda Mlango Juma Kaseja wakisema kuwa wapo tayari kwa mtanange huo.

Taifa Stars itamenyana na Equatorial Guinea hapo kesho saa moja usiku, kwenye dimba la Taifa jijini Dar es salaam, ukiwa ni mchezo wa kwanza wa kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2021 zitakayofanyika nchini Cameroon.