Stars, Tanzanite, Yanga, Azam na Malindi zapongezwa

0
1322

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameipongeza Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu (Taifa Stars)kwa kuziondosha Harambee Stars ya Kenya na Burundi kwenye hatua za awali za kusaka tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia na CHAN na hivyo kusonga mbele katika hatua inayofuata ya michuano hiyo.

Waziri Mkuu pia ameipongeza Timu ya Taifa ya Wanawake wenye umri wa chini ya miaka Ishirini (TANZANITE) kwa kuibuka mabingwa wa michuano ya COSAFA yaliyofanyika mwaka huu huko Afrika Kusini.

Katika pongezi hizo Waziri Mkuu Majaliwa ameipongeza klabu ya soka ya Yanga, Azam na Malindi kwa kufanikiwa kusonga mbele kwenye hatua ya pili ya michuano ya klabu Bingwa Barani Afrika na Kombe la Shrikisho.

Pongezi hizo zimetolewa hii leo na Waziri Mkuu Majaliwa wakati akisoma hotuba ya kuahirisha mkutano wa 16 wa Bunge jijini Dodoma.

Waziri Mkuu pia amewapongeza Wana Masumbwi wa Tanzania Abdalah Pazi maarufu kama Dula Mbabe kwa kuibuka Bingwa wa Dunia wa Mkanda wa WBO na Bruno Tarimo kwa kuibuka na ushindi katika pambano la ubingwa wa Dunia.

Waziri Mkuu pia amemtakia kila la kheri Mrembo wa Tanzania, – Sylvia Bebwa katika shindano la Urembo la Dunia, linalotarajiwa kufanyika nchini Uingereza Disemba 14 mwaka huu.