Stars kucheza na Rwanda Oktoba 14

0
1068

Timu ya Taifa ya Soka ya Tanzania (Taifa Stars), itacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Rwanda Oktoba 14 mwaka huu kwenye uwanja wa Kigali nchini Rwanda.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeeleza kuwa, mchezo huo utakuwa kwenye tarehe za kalenda ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani(FIFA) na tayari imeshafikia makubaliano na Shirikisho la Soka la Rwanda.