Simba vs KMC hakuna mbabe

0
204

Timu ya Simba imetoka sare ya 2-2 na watoza ushuru wa Kinondoni KMC katika mechi iliyopigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Magoli ya SIMBA yamefungwa na Mosses Phiri na Habib Kyombo huku magoli ya KMC yakifungwa na Matteo Anthony na George Makang’a.

Kwa matokeo SIMBA anafikisha alama saba huku KMC wakiongeza alama nyingine moja kwenye msimamo.

Mapema leo Klabu ya Mtibwa Sugar imepata Ushindi mzito katika dimba la nyumbani Manungu Turiani mkoani Morogoro kwa kuwafumua Mbogo Maji Ihefu Fc magoli matatu kwa moja.

Magoli ya Mtibwa yamefungwa na Ismail Mhesa, Issa Rashid na Nickson Kibabage huku goli la kufutia machozi la Ihefu likifungwa na Andrew Simchimba.

Kwa matokeo hayo Mtibwa Sugar inafikisha alama saba huku Ihefu ikiendelea kusalia mkiani bila kuwa na alama yoyote