Simba yawasha moto Tabora

0
3057

Klabu ya Simba imeipa Klabu ya soka ya KMC kipogo cha mabao 4-1 katika mchezo wa Ligi kuu ya NBC ambayo ipo katika mzunguko wake wa 10.

Mchezo huo wa ligi kuu ya NBC umechezwa kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Mjini Tabora ambapo KMC imeutumia kama uwanja wake wa nyumbani katika mchezo wa leo.

Simba ilianza kupata bao la mapema kabisa kupitia kwa Beki wao kisiki Mohammed Hussein katika dakika ya 10 na baadae bao la pili likifungwa na Joash Onyango akaongeza la pili dakika ya 13.

Mabao mengine mawili kwa Simba yamefungwa katika kipindi cha pili na kiungo wake mshambuliaje Kibu Denis.

Bao la kufutia machozi kwa KMC limefungwa katika kipindi cha kwanza na Abdul Hassan katika dakika ya 39 ya mchezo huo