Simba yatinga hatua ya 16 bora ASFC

0
199

Wekundu wa Msimbazi Simba imefanikiwa kutinga hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la Azam sports.

Simba imefanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kuitandika Afrikan Lyon mabao 3 kwa bila katika mchezo ulipigwa kwenye dimba la Mkapa mkoani Dar es Salaam.

Mabao ya Simba katika mchezo huo yamefungwa na Ibrahim Ajib ambaye amefunga mabao mawili na Parfect Chikwende aliyefunga bao la 3 katika dakika ya 63 ya mchezo huo