Simba yamtambulisha Mohamed Ouattara

0
142

Klabu ya soka ya Simba imemtambulisha Mchezaji Raia wa Ivory Coast Mohamed Ouattara katika kikosi cha msimu ujao cha timu hiyo.

Ouattara amehamia Simba akitokea klabu ya Al Hilal ya Sudan ikiwa ni mapendekezo ya kocha Zoran Maki ambaye amewahi kufanya kazi na Mchezaji huyo ambaye ni mlinzi wa kati.

Katika kurasa zake za mitandao ya kijamii klabu ya Simba imemtambulisha mchezaji huyo kwa kuandika maneno yanayosomeka “Beki kisiki, beki wa kuzuia mipira ya juu na chini, beki bora na mwenye uwezo wa kucheza kwenye kikosi chetu. Mohamed Ouattara”