Simba yaendelea kujikita kileleni, Yanga yavutwa shati Taifa

0
348

Klabu ya Simba ya jijini Dar es salaam imeibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya timu ya Mtibwa SugarĀ  ya mjini Morogoro na kuifanya kufikisha alama 53 na hivyo kuendelea kujikita kileleni mwa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mchezo kati ya Simba na Mtibwa umechezwa katika uwanja wa Jamhuri uliopo mjini Morogoro ambapo mashabiki walijitokeza kwa wingi kushuhudia mchezo huo uliokuwa na ufundi wa kila aina.

Mabao ya Simba yalifungwa na nahodha John Bocco, Mohammed Hussein na bao la tatu lilifungwa na Hassan Dilunga.

Ushindi wa Simba umerejesha matumaini ya timu hiyo kufanya vizuri ambapo timu hiyo iliingia uwanjani ikiwa imetoka kupoteza mchezo wao uliopita dhidi JKT Tanzania walioshinda bao 1-0

Upande wa Mchezo wa Yanga dhidi ya Mbeya City mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa Dar es salaam umemalizika kwa sare ya bao moja kwa moja.