Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limetoa orodha ya viwango vya ubora baada ya mashindano ya shirikisho hilo kwa msimu wa 2022/23 ambapo Simba SC imeshika nafasi ya tisa, huku Yanga SC ikiwa ya 18.
Katika msimu huo Simba ilikusanya alama tatu baada ya kufika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa, na hivyo kufikisha jumla ya alama 35 huku Yanga ikikusanya alama 4 kwa kufika Fainali ya Kombe la Shirikisho na hivyo kufikisha jumla ya alama 20.
Hapa chini ni orodha ya vilabu 10 bora zaidi kwa mwaka 2022/23;
- Al Ahlly SC
- Wydad AC
- Espérance Sportive de Tunis
- Mamelodi Sundowns F.C.
- Raja CA
- Zamalek SC
- RS Berkane
- CR Belouizdad
- Simba SC
- Pyramids FC
Katika orodha hii Misri na Morcco zinaongoza kila moja ikiwa na vilabu vitatu.