Sharapova atangaza kustaafu tenisi

0
451

Bingwa wa tenisi wa mataji matano ya Grand Slam kwa upande wa Wanawake, Maria Sharapova, ametangaza kustaafu mchezo huo akiwa na umri wa miaka 32.

Sharapova amesema mwili wake umekuwa kikwazo kikubwa baada ya kupambana kwa muda mrefu, pamoja na jeraha la bega lililokuwa likimuweka nje ya uwanja muda mrefu.

Mrussia huyo alishinda taji lake la kwanza lenye hadhi ya Grand Slam katika mshindano ya Wimbledon mwaka 2004 akiwa na umri wa miaka 17, na Grand Slum yake ya mwisho alishinda mwaka 2012 katika mashindano ya wazi ya Ufaransa.

Hata hivyo mwaka 2016 alifungiwa kwa muda wa miezi 15 baada ya kukumbwa na kadhia ya matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku michezoni na baada ya kumaliza adhabu hiyo amekuwa akipambana kurejea katika ubora wake bila mafanikio.

Sharapova alizaliwa Aprili 19 mwaka 1987 huko Nyagan, Russia.