Katibu Mkuu wa wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi amesema Serikali imejipanga kuisaidia timu ya Taifa ya soka (Taifa Stars), kwa kuipatia fedha ili kuongeza ufanisi wa timu hiyo.
Dkt. Abbasi amesema hayo mkaoni Dar es salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Katibu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Kidao Wilfred.
Wakati wa mazungumzo yao, Dkt. Abbasi na Kidau wamejadili namna ya kuiwezesha Stars kwenye maandalizi ya michuano ya awali ya kufuzu kombe la Dunia yanayotarajiwa kufanyika mwezi Juni hadi Agosti mwaka huu.
“Ili kupata matokeo mazuri wachezaji wetu lazima wawe vizuri kifedha, hii itawasaidia kisaikolojia kuweza kupata matokeo mazuri.” Amesema Dkt. Abbasi.
Kwa upande wake Kidao amesema maandalizi yote yamekamilika, huku akieleza kuwa changamoto iliyobaki ni ukosefu wa fedha ambapo ameshukuru namna Serikali inavyojipanga kukabiliana na changamoto hiyo.