Serengeti Girls yafuzu kuingia robo fainali

0
1054

Timu ya wasichana ya Tanzania wenye umri wa chini ya miaka 17 (Serengeti Girls), imefuzu kuingia robo fainali za Kombe la Dunia baada ya kutoka sare ya 1-1 na Canada, katika mchezo wa mwisho wa kundi D kwenye mashindano ya Kombe la Dunia kwa umri huo.

Mchezo huo umepigwa katika dimba la DY Patil Navi – Mumbai nchini India.