Timu ya Taifa ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 (Serengeti Boys) inaendelea na kambi yake jijini Arusha, kujiandaa na fainali za vijana za AFCON zitakazofanyika nchini kuanzia Aprili 14 mwaka huu.
Kikosi cha timu hiyo kinajifua katika viwanja vya AGHAKHAN jijini Arusha kikiwa na morali ya hali juu, ambapo kabla ya kushiriki fainali hizo za AFCON, vijana hao watashiriki mashindano maalum ya UEFA ASSISTS yatakayofanyika Antalya nchini Uturuki kuanzia Machi Mosi hadi Tisa mwaka huu kwa mwaliko maalum wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Ulaya (UEFA).
Mashindano hayo maalum yameandaliwa na UEFA kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) na yanashirikisha timu 12.
Serengeti Boys imepangwa kundi A ikiwa na timu za Guinea, Uturuki na Australia.