Senegal yamuongezea kandarasi Cise

0
120

Chama cha soka nchini Senegal kimemuongezea mkataba wa kuendelea kukinoa kikosi cha timu ya Taifa ya nchi hiyo kocha Aliou Cise mpaka mwaka 2024.

Cise ambaye ni nahodha wa zamani wa Senegal ameingezewa pia mshahara kutoka Dola za marekani elfu 23 za sasa mpaka Dola elfu 40 kwa mwezi.

Kocha huyo ameiwezesha Senegal almaarufu Simba wa Teranga kutwaa ubingwa wa Afrika mwaka huu na pia kufuzu kwa fainali za kombe la FIFA la Dunia 2022 huko Qatar.