Samatta kuukosa mchezo wa Tunisia

0
266

Nahodha wa Timu ya Taifa ya soka ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Mbwana Samatta, atakosa mchezo wa kufuzu michuano ya Afrika dhidi ya Tunisia kutokana na kuwa majeruhi.

Akiongea na TBC Online toka nchini Uturuki ilikoweka kambi Taifa Stars, Kocha mkuu wa timu hiyo Etinne Ndayiragije amesema Samatta aliumia akiwa na timu yake ya Fenerbahçe, na atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa wiki mbili hivyo hawezi kucheza mchezo wa ijumaa dhidi ya Tunisia.

Taifa Stars itacheza na Tunisia mchezo wa mkondo wa kwanza wa kufuzu kwa michuano ya AFCON siku ya ijumaa huko Tunisia na kurudiana hapa nchini Novemba 17 ya mwaka huu kwenye dimba la Benjamin Mkapa.