Taarifa ya kocha wa Aston Villa kuhusu usajili wa Samatta

0
924

Kocha wa timu ya Aston Villa, Dean Smith amethibitisha kwamba mpango wao wa kumsajili nyota wa Kitanzania Mbwana Samatta utakamilika hivi karibuni

Akizungumza baada ya mechi yao ya jana dhidi ya Brighton ambayo ilimalizika kwa timu hizo kwenda sare kwa kufungana bao moja kwa moja, kocha huyo amesema kila kitu kimeenda vizuri na Mbwana Samatta alikuwa akikamilisha kusaini nyaraka zilizokuwa zimesalia.

Kocha Smith amesema Samatta ni mshambuliaji bora na atakuwa na msaada mkubwa kwao kutokana na rekodi yake nzuri ambapo alifunga magoli 43 katika michezo 98 kwenye ligi ya Ubelgiji alipokuwa akiichezea timu ya KRC Genk.