SAMATTA KUCHUANA NA AKINA MANE, MO SALAH TUZO YA MCHEZAJI BORA AFRIKA

0
995

Nahodha wa #TaifaStars anayesakata kabumbu katika timu ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta ametajwa katika orodha ya wachezaji 30 wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika mwaka 2019.

Katika orodha hiyo iliyotolewa leo na Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) wamo pia Mohamed Salah wa Misri (Liverpool), Piere-Emerick Aubameyang wa Gabon (Arsenal), Sadio Mane wa Senegal (Liverpool) na Riyad Mahrez wa Algeria (Manchester City). Sherehe za tuzo hizo zitafanyika Januari 7, 2020 nchini Misri.