Samatta Awafunga Liverpool

0
1101

Nahodha wa Taifa Stars na Mshambuliaji wa Kimataifa anaekipiga Klabu ya KRC Genk ameendelea kung’ara katika Michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kufunga bao moja dhidi ya Mabingwa Watetezi wa Taji Hilo Liverpool dakika ya 41

Licha ya Samatta kufunga bao hilo timu yake Genk imepoteza mchezo huo kwa kutandikwa mabao mawili kwa moja

Mabao ya Liverpool yamefungwa mapema na mchezaji Wijnaldum dakika 14 huku Chamberlain akipigilia msumari wa pili dakika ya 53 na kufanya matokeo kuwa 2 kwa moja hadi dakika 90

Kwa matokeo hayo Liverpool inaendelea kuongoza kundi E kwa alama 9 huku Genk ikishika mkia na alama moja