Mshambuliaji wa timu ya Liverpool na timu ya Taifa ya Misri Mohmed Salah ametangazwa na Shirikisho la soka Barani Afrika Caf kuwa mchezaji bora wa mwaka 2018 wa Afrika katika sherehe za utoaji wa tuzo zilizofanyika jijini dakar nchini senegal
Mohamed Salah amewashinda nyota wengine waliokuwa wanawania tuzo hiyo, Sadio Mane wa Liverpool pamoja na Pierre-Emerick Aubameyang wa Arsenal ambao wanacheza ligi kuu ya England.
Wakati huo huo shirikisho la soka Barani Afrika Caf limeiteua nchi ya Misri kuandaa fainali za Mataifa ya Afrika zitakazofanyika Juni mwaka huu.
Taifa hilo la Kaskazini mwa Afrika lina miezi isiyozidi sita ya kujiandaa kwa fainali hizo zitakazoshirikisha mataifa 24 mwaka huu.
Misri inaandaa fainali hizo baada ya shirikisho la soka Afrika (Caf) kuipoka Cameroon uenyeji wa fainali hizo kutokana na kusuasua kwa maandalizi ya fainali hizo.