Ruvu Shooting yaipapasa Coastal Union uwanja wa Uhuru

0
586

Ruvu Shooting FC wenyewe wakijiita Wazee wa Mpapaso au Barcelona ya Bongo imepata ushindi wa tatu katika michezo mitano ya Ligi Kuu ya NBC baada ya kuwaadhibu Wagosi wa Kaya, Coastal Union FC kwa magoli 2-1.

Coastal Union ndio walikuwa wa kwanza kupata goli katika dakika za mapema kabla ya Ruvu Shooting kuweka sawa mizani hadi kipindi cha kwanza kinamalizika.

Kipindi cha pili timu hiyo kutoka mkoani Pwani ilipata goli la pili na la ushindi kupitia kwa mfungaji wa goli la kwanza, Rashid Juma.

Kwa ushindi huo Wazee wa Mpapaso wanapanda hadi nafasi ya tano wakiwa na alama tisa, huku Coastal Union wakiwa katika nafasi ya 12 wakiwa na alama nne katika michezo mitano.

Coastal imeshinda mchezo mmoja tu, huku ikitoka sare mmoja na kupoteza michezo mitatu, wakati Ruvu Shooting wao wameshinda michezo mitatu na kupoteza miwili.