Ronaldo njia panda Saudia Arabia

0
177

Nyota wa Ureno, Cristiano Ronaldo na mchumba wake, Georgina huenda wasiishi pamoja nchini Saudia Arabia kutokana na sheria za nchi hiyo kukataza watu ambao hawajafunga ndoa kuishi pamoja.

Taifa la Saudia Arabia linafuata sheria za Kiislamu na hivyo sheria hizo zinambana moja kwa moja Ronaldo na mchumba wake.

Hata hivyo, kwa mujibu wa Jarida la EFE, Ronaldo hatoathiriwa na sheria hiyo kwa kuwa wanamtazama kama ‘Mfanyakazi’ aliyekwenda kuitangaza nchi yao. Lakini bado Wahafidhina wanasisitiza Ronaldo amuoe Georgina ili maisha yaendelee.