Ronaldo kulipa fadhila

0
1192

Nyota wa Juventus na Timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo ametangaza kuwa anamtafuta Mwanamke aliyemtaja kwa Jina la Edna pamoja na Wanawake wengine wawili waliomsaidia alipokuwa hajulikani na hana kitu kwa kumpa Chakula aina ya burger zilizobaki kwenye Mgahawa wa MacDonald kipindi akiwa na Miaka 11 huko Lisbon Nchini Ureno.

Baada ya Mgahawa kufungwa, Ronaldo amekuwa akiwatafuta bila kuwapata Wanawake hao Watatu ambao ni ‘Edna’ pamoja na wengine Wawili ili alipe fadhila na kuwashukuru kwa kile walichomfanyia kwa kipindi kile.

Je mara ngapi umekumbuka kulipa fadhila?na ukafanikisha?