Ronaldo bado alitamani kombe la Dunia

0
142

Mshambuliaji wa klabu ya Juventus  na raia wa Ureno Cristiano Ronaldo anasema ana matumaini ya kuendelea kucheza kwa miaka mingi lakini ndoto yake kubwa ni kutwaa kombe la dunia.

Ronaldo, mwenye miaka 35 anahitaji mabao saba tu ya kimataifa ili aweze  kufikia  rekodi ya dunia ya kufikisha  mabao 109 kama rekodi iliyowekwa na mchezaji Ali Daei wa Iran.

Ronaldo anasema huu ni mpira wa miguu, hatujui ni nini kitatokea kesho na anasema mara nyingi anapozungumza na vijana wadogo anawaambia furahia wakati huu kwa sababu hujui nini kitatokea kesho.

Kazi ya Ronaldo ilianza huko Sporting, ambapo alicheza mechi 31 kutoka 2002 hadi 2003 kabla ya kuhamia Manchester United, ambapo alicheza mechi  292 na Man u , alijiunga na Real Madrid mnamo 2009 na alibaki huko hadi 2018 kisha akajiunga na klabu ya Juventus ya Italia.