Ronaldo aweka rekodi nyingine duniani

0
261

Katika mchezo kati ya Ureno na Liechtenstein, Cristiano Ronaldo ameweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyecheza michezo mingi ya timu ya Taifa duniani.

Mchezo huo ambao alifunga magoli mawili katika ushindi wa 4-0, ulishuhudia Ronaldo akicheza mchezo wa 197 kwa Taifa akimpita Bader Al-Mutawa wa Kuwait mwenye michezo 196.

Mbali na hilo, nyota huyo wa Al Nassr ya Saudia amefikisha magoli 119, akiongoza kwa mchezaji mwenye magoli mengi wa kimataifa.

“Napenda kuvunja rekodi, nimevunja rekodi nyingi sana,” amenukuliwa na waandishi habari kuelekea mchezo huo ambao ulikuwa wa kwanza kwa kocha Roberto Martinez.