Ronaldo avunja ukimya baada ya kutolewa Kombe la Dunia

0
740

Mshambuliaji wa Ureno, Cristiano Ronaldo amesema ndoto yake kubwa na muhimu zaidi ilikuwa kuiwezesha Ureno kushinda Kombe la Dunia, na kwamba licha ya kuwa kwa pamoja wameweza kushinda makombe mengi, lakini kushinda taji hilo ilikuwa ni ndoto yake kubwa zaidi.

Siku moja baada ya kutolewa katika mashindano hayo kufuatia kufungwa na Morocco goli 1-0, Ronaldo amesema ni wazi sasa kuwa ndoto aliyoipigania kwa miaka mingi ya kuiwezesha Ureno kushinda Kombe la Dunia, sasa rasmi imekufa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ronaldo amesema, katika mara 5 alizoshiriki mashindano hayo alipambana sana kwa kushirikiana na wenzake na kwamba hakuwahi kukata tamaa kuhusu kufanikisha ndoto hiyo.

“Kwa huzuni, jana ndoto hiyo ilizimwa,” ameeleza akisisitiza kwamba licha ya kuwa mengi yamesemwa kumhusu, lakini kujitoa kwake kwa Ureno hakujawahi kubadilika.

Haya ndio yalikuwa mashindano ya mwisho ya Kombe la Dunia kwa Ronaldo ambaye ana umri wa miaka 37.