Ronaldo atua Al Nassr

0
207

Klabu ya Al Nassr ya Saudi Arabia imethibitisha kumsajili gwiji wa soka raia wa Ureno, Cristiano Ronaldo kwa mkataba unaodumu hadi mwaka 2025.

Habari za kusajiliwa kwake zimethibitishwa Ijumaa usiku na klabu hiyo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Klabu imeandika “Mwanasoka mkubwa zaidi duniani amesainiwa rasmi,” ujumbe ulioambatana na picha za Ronaldo akiwa ameshikilia jezi ya Al Nassr.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 aliondoka Manchester United baada ya kusitishwa kwa kandarasi yake mwezi Novemba na amekuwa mchezaji huru tangu wakati huo baada ya kutofautiana na klabu hiyo kutokana na kushindwa kuhama msimu wa joto na mahojiano aliyoyafanya na mtangazaji maarufu Piers Morgan na kuzua taharuki kati yake na waajiri wake.