Ronaldo aingia katika rekodi za Guinness

0
2263

Christiano Ronaldo ambaye ni.mchezaji wa klabu.ya Manchester United ya nchini Uingereza, ametunukiwa Tuzo ya kutambua rekodi yake ya kuwa mfungaji bora wa kimataifa (Guiness Records).

Ronaldo ametunikiwa Tuzo hiyo baada ya kuweka rekodi hiyo kwa kufunga magoli mengi kwenye mechi za kimataifa

Ronaldo ameweka rekodi hiyo baada ya kufunga mabao mawili Kwenye mechi ya kuwania kufuzu fainali za kombe la FIFA la Dunia kati ya Jamhuri ya Ireland dhidi ya Ureno.

Awali rekodi hiyo iliuwa ikishikiliwa na Ali Daiei wa Iran kwa kufunga mabao 109, lakini Ronaldo ameivunja kwa kufikisha jumla ya magoli 111 tangu alipoanza kucheza soka la kimataifa mwaka 2003.