Ronaldo acheza mchezo wa elfu moja

0
453

Cristiano Ronaldo amecheza mchezo wa elfu moja tangu aanze kusakata kandanda katika ushindi wa mabao mawili kwa bila waliopata Juventus dhidi ya Inter Milan nchini Italia.

Ronaldo alianza maisha yake ya soka katika klabu ya Sporting Lisborn ya nyumbani kwao Ureno, akiitumikia katika michezo 31 na kuifungia mabao matano kabla ya kutimkia Manchester United ambapo alicheza michezo 292 na kufunga mabao 118.

Baada ya hapo alijiunga na Real Madrid, ambapo alicheza michezo 438 na kufunga mabao 450, kisha akajiunga na Juventus ambayo mpaka sasa ameichezea michezo 75 na kuifungia mabao 53 huku akifunga mabao mengine 99 katika michezo 164 aliyoitumikia timu yake ya Taifa ya Ureno mpaka sasa.

Kiujumla Ronaldo amefunga mabao 725 katika michezo elfu moja aliyocheza mpaka sasa, huku akishinda mataji matano ya ligi tofauti, mataji matano  ya ligi ya mabingwa Barani Ulaya, tuzo ya mwanasoka bora wa dunia ya Ballon d’Or mara tano  na ubingwa wa mataifa ya Ulaya mara moja.