Rais wa China Xi JinPing amezindua rasmi mashindano ya Dunia ya Majeshi katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Michezo katika jiji la wuhan.
Mbali na kuwataka wanamichezo kutumia michezo hiikujenga urafiki badala ya uadui na kuwataka wanamichezo wawe na matendo ya kiungwana.
Uzinduzi huo uliambatana na halaiki na michezo mbali ikiwemo flashflash na burudani kutoka kwa wasanii mahiri akiwemo mcheza cinema Jack Chain aliyetoa burudani kwa kuimba.
Akizungumza mara baada ya uziduzi huu mkurugenzi wa michezo jeshini na mkuu wa msafara msaidizi Kanali Erasmus Bwegoge amesema uzinduzi umefana na Timu ya Ngumi ndio itaanza michezo yake kesho
Kwa upande wa mabondia Selemani Kidunda ,alex Isendi na Ismail Galiatano wakati wakujiandaa na michezo hiyo wamesema wako safi na tayari kwa mashindano
@tbc_michezo #tbc_online
