Rais Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wametoa tiketi 4,000 kwa ajili ya mashabiki kuingia uwanja wa Benjamin Mkapa katika mchezo kati ya Tanzania na Uganda.
Katika mchezo huo utakaopigwa Machi 28 mwaka huu mkoani Dar es Salaam, mataifa haya kutoka Afrika Mashariki yatarudiana ikiwa ni michezo ya hatua ya kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2023.
Akizungumza kwa njia ya simu, Waziri Mkuu Majaliwa amesema uamuzi wa kutoa tiketi hizo ni kuendeleza mkakati wa Rais wa kukuza ari ya michezo nchini, kama ambavyo amefanya kwa vilabu vya Simba na Yanga.
Awali, Rais Samia aliahidi kutoka TZS milioni 500 endapo timu hiyo itafuzu mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika nchini Ivory Coast kuanzia Januari 2024.
Timu hizo zitashuka dimbani kesho nchini Misri katika mchezo wa kwanza, kila timu ikiwania alama tatu muhimu.