Rais Magufuli afurahia ushindi wa stars

0
443

Rais John Magufuli ameipongeza Timu ya Taifa ya Soka (Taifa Stars) kwa kufuzu kucheza fainali za michuano ya Afrika kwa mwaka 2019.

Rais Magufuli ambaye alikuwa akifuatilia pambano hilo kupitia Luninga, amerekodiwa picha ya video akifurahia ushindi baada ya pambano la Taifa Stars na Timu ya Taifa ya Uganda (The Cranes) kumalizika kwa Taifa Stars kupata ushindi wa magoli 3 kwa 0.

Rais Magufuli amesema kuwa ushindi huo ni heshima kubwa kwa nchi na amewapongeza Watanzania wote kwa kufanikiwa kupeleka timu yao ya Taifa katika fainali za AFCON ikiwa ni miaka 39 tangu ilipofanikiwa kufika hatua hiyo mwaka 1980.

Mchezo wa Taifa Stars na The Cranes umefanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.