PSG yatinga fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya

0
324

PSG usiku wa kuamkia leo imefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya baada ya kuitandika RB Leipzig ya Ujerumani kwa mabao 3-0

Mchezo huo wa hatua ya nusu fainali umepigwa Mjini Lisbon nchini Ureno na umekuwa na ushindani mkubwa lakini mwisho wa siku PSG wakaibuka wababe na kufanikiwa kusonga mbele.

Kipindi cha kwanza PSG ilitupia mabao mawili ambapo bao la kwanza lilipachikwa na Marquinhos dakika ya 13 na Angel Di Maria akafunga bao la pili dakika ya 42 na bao la tatu na la mwisho lilipachikwa na Benatti dakika ya 56.

Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya inatarajiwa kuchezwa Jumapili, Agosti 23 ambapo leo usiku wababe Bayern Munich wataumana na Olympic Lyon ya Ufaransa katija mchezo wa nusu fainali ya pili, na mshindi atakipiga na PSG kupata bingwa wa fainali hizo.